Michezo

Man City waanza kupewa presha ya Ubingwa wa EPL, point 8 za Liverpool juu yao

on

Presha kwa Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu ya England Man City kuweza kutetea taji hilo inazidi kuwa kubwa kufuatia tofauti ya point iliyopo kati yake na wapinzani wake wakubwa Liverpool ambao tayari wamejikita kileleni kwa tofauti ya point 8 (24) huku Man City wakifuatia kwa kushika nafasi ya pili kwa point 16.

Kufuatia presha hiyo mshambuliaji wa zamani wa Ireland Tony Cascarino akiongea na TalkSport amewapa onyo Man City kuwa tofauti hiyo ya point inaweza kuongezeka zaidi wasipokuwa makini, ukizingatia beki wao wa kati yupo nje ya uwanja Aymeric Laporte kwa majeruhi hadi mwanzoni mwa 2020 kitu kinacholazimika Fernandinho kucheza nyuma huku Kevin De Bruyne nae akiwa nje kwa tatizo la groin.

“Ni wazi Kevin De Bruyne na Aymeric Laporte ni wachezaji muhimu sana wanatakiwa wawe makini na utofauti wao wa point kwa sababu naona Liverpool wamekuwa wakiongeza kufanya vizuri katika miezi ijayo, sioni Man City wakiwasogelea, sio kama msimu uliopita msimu uliopita Man City walikuwa wazuri zaidi lakini sasa hivi sio kama mwaka ulioisha huenda kwa sababu ya majeruhi”>>>Tony Cascarino

Msimu uliopita timu za Man City na Liverpool ndio walikuwa washindani wa karibu wa kuwania taji la Ligi Kuu England lakini sasa hivi kila mmoja wao amecheza michezo nane Liverpool akishinda mechi zote na kuwa na point 24 wakati Man City wao wakiwa wameshinda michezo 5 kati ya nane waliocheza, wamepoteza michezo 2 na sare mchezo mmoja.

VIDEO:AJIB BWANA MIPANGO !!! KAANZISHA MOVE NA KWENDA KUFUNGA

Soma na hizi

Tupia Comments