Mama wa Joycelyn Savage ( mmoja wa Wapenzi wa R. Kelly) amezungumza mbele ya vyombo vya habari na kuomba kukutana na mwanae baada ya kupita miaka miwili bila kuonana hii ni baada ya Mwanae huyo kumtuhumu yeye pamoja na Mume wake kumtishia Mwimbaji R. Kelly ili wajipatie fedha.
kupitia mahojiano ya kituo cha TV cha CBS “This Morning” kilifanya mahojiano na wasichana wawili ambao walitajwa kuwa waliwahi kuwa mapenzini na mwimbaji R. Kelly na kusema kuwa wazazi wao waliwataka wadanganye kuhusu umri wake pamoja na kutengeneza kanda za ngono pamoja na R.Kelly ambapo baadae wangezitumia kwa kulipiza kisasi.
Jocelyn Savage pamoja na Azriel Clary walisisitiza na kusema kuwa wazazi wao waliwataka wafanye hivyo ili baadae watumie picha pamoja na videos hizo kama ushahidi endapo R.Kelly angegoma kutoa kiasi cha pesa walichokitaka huku lengo lao kubwa ilikua kukusanya pesa kutoka kwaR. Kelly .
“Tunachotaka kujua ni kama Mtoto wetu yupo sawa kiakili na kimwili na hafayiwi unyanyasaji wowote lakini tusiposkia chochote kutoka kwake kwa siku moja au wiki basi tunajua una kitu kibaya basi tutaomba team ya R.Kelly kuoma kukutana na mtoto wetu” >>> Mama wa Jocelyn Savage
VIDEO: “Naishi comfortable life mimi siyo mtu wa kiki, nataka kusaidia models wachanga” Miriam Odemba