Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika club ya Juventus ya Ureno Cristiano Ronaldo anaweza kujikuta akiingia matatizoni na chama cha soka Ulaya UEFA, kufuatia kuanza kuchunguzwa kwa aina ya style ya ushangiliaji iliyokuwa gumzo.
Ronaldo ambaye aliifungia Juventus magoli matatu (hat-trick) 3-0 dhidi ya Atletico Madrid katika come back 2-0 waliyofungwa katika mchezo wao wa kwanza wa 16 bora ya UEFA Champions League, amefunguliwa mashitaka na kuanza kuchunguzwa na UEFA kutokana na style yake hiyo.
Cristiano Ronaldo anadaiwa style yake ya ushangiliaji aliyomuiga kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone katika mchezo wa kwanza waliokuwa wamepoteza 2-0, haina tafsiri nzuri hivyo kama ikibainika ililenga kudhihaki wapinzani wao anaweza kufungiwa.
Hata hivyo Diego Simeone ambaye ndio alianza kushangilia kwa style kama hiyo ambayo imedaiwa kuwa Ronaldo ameifanya ili kulipa kisasi, nae anachunguzwa na amefungiliwa mashitaka kwa na UEFA na wakijiridhisha Cristiano Ronaldo na Diego Simeone watakumbana na adhabu kutoka UEFA, ambapo itakuwa pigo kwa Ronaldo anayeweza kuikosa robo fainali dhidi ya Ajax.
Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!