Michezo

FIFA imekata mzizi wa fitna ishu ya kufungiwa maisha Wambura

on

Baada ya kamati ya maadili ya shirikisho la soka Tanzania TFF kumfungia maisha kujihusisha na soka aliyekuwa makamu wao wa Rais wa Shirikisho hilo Michael Richard Wambura, Wambura aliamua kwenda Mahakamani kupinga maamuzi hayo ambapo inaelezwa kuwa alishinda kesi.

December 4 2018 Wambura aliwasili TFF na hati ya Mahakama iliyotengua uamuzi wa TFF kumfungia maisha kujihusisha na soka, Wambura alieleza kuwa Mahakama Kuu walifikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa kumekiukwa baadhi ya taratibu.

Hata hivyo Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetoa taarifa mpya kutoka shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA ikieleza kuwa imetangaza pia kumfungia maisha ya kujihusisha na soka Michael Richard Wambura.

Kauli ya Wambura aliyoitoa December 4 2018 “Tumekuja hapa kukabidhi maamuzi ya Mahakama Kuu Tanzania ya kupinga maamuzi ya kamati za TFF, mwezi uliopita Mahakama Kuu ilitengua maamuzi ya mimi kufungiwa kushiriki soka kwa maana hiyo baada ya maamuzi yale tarehe 30 naendelea kuwa Makamu wa Rais wa TFF”

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments