Michezo

El Clasico ya FC Barcelona na Real Madrid imeahirishwa

on

Mechi ya El Clasico iliyokuwa inazikutanisha timu za FC Barcelona dhidi ya Real Madrid iliyotarajiwa kuchezwa Octobe 26 2019 katika uwanja wa Nou Camp Catalunya jijini Barcelona imeahirishwa, mechi hiyo imeahirishwa  kwa sababu za kiusalama.

Game hiyo ya El Clasico imeahirishwa kwa sababu za machafuko ya kisiasa yanayoendelea katika jimbo la Catalunya, club za Real Madrid na FC Barcelona zimepanga kukutana na Jumatatu na kujadiliana ni lini itachezwa mechi hiyo.

Mwanzo ilipendekezwa mchezo huo ukachezwe katika dimba la Santiago Bernabeu katika jiji la Madrid, ila kocha wa Barcelona Ernest Valverde amekataa mchezo huo kuamishiwa Madrid kwa sababu itakuwa inaenda kuchezwa siku 3 ikiwa wametoka October 23 kucheza dhidi ya Slavia Prague hivyo wachezaji watakuwa wamechoka.

AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments