Habari za Mastaa

Soulja Boy adai aliyeiba nyumbani kwake ni mtu wake wa karibu

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ uliyoripoti kuwa nyumba ya Rapper Soulja Boy iliyopo mjini California Marekani, ilivamiwa na wezi na kuondoka  vitu vya thamani ikiwemo pesa, vitu binafsi na simu ya mkononi aina ya iPhone ambayo waliitumia kwenda Insta LIVE kwenye instagram yake mwenyewe wakati wakifanya tukio hilo.

Inadaiwa kuwa thamani ya vitu hivyo vilivyoibiwa vinatajwa kufikia thamani ya Tsh Bilioni 1 za Kitanzania huku kiasi cha pesa taslimu kilichoibiwa ni zaidi ya Tsh Milioni 200 za Kitanzania, kwa mujibu wa Soulja Boy amedai kuwa anaamini wezi hao hawajatoka mbali bali ni watu ambao wanamzunguka yaani washkaji zake.

Inaripotiwa kuwa rapper Soulja Boy kwa sasa bado yupo jela akisubiri kusikilizwa kwa shauri lake la kuvunja masharti ya muda aliyopewa chini ya uangalizi (Probation), hivyo wezi wakaitumia hiyo kama fursa ya kwenda kufanya uhalifu na kuiba katika nyumba ya rapper huyo.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA WAKAZI? ‘SILAZIMISHI / SI-FORCE, ACHA MUZIKI UONGEE’

Soma na hizi

Tupia Comments