AyoTV

EXCLUSIVE: Usiyoyajua kuhusu Haji Manara wa Simba, Baba mzazi kaongea

on

Afisa habari wa Simba SC Haji Manara ni moja kati ya watu maarufu sana katika michezo kwa sasa lakini pengine hujui kama Haji Manara ametokea katika familia ya mpira, kingine kilichomfanya Haji Manara kuwa maarufu sana ni hali yake ya kujiamini zaidi ukilinganisha na hali yake ya ulemavu wa ngozi ‘Albino’ ambapo wengine huwa wanajitenga na kuhisi kama ndio basi tena kwenye haya maisha.
So Leo nakukutanisha na baba mzazi wa msemaji wa Simba Haji Manara anayejulikana kwa jina la Sunday Ramadhan Manara ambaye ameeleza kuwa Haji Manara alianza kujiamini tangia utotoni na amewahi kumletea mashekh nyumbani na kumuamsha na kumshitaki kwa mashekh kuwa baba yangu mimi hasali.
Kama humfahamu vizuri mzee Sunday Ramadhan Manara aliyezaliwa miaka 65 iliyopita mkoani Kigoma aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga SC na timu ya taifa ya Tanzania lakini pia ni miongoni mwa wachezaji wachache mno waliowahi kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya bara la Afrika.
Sunday Manara amewahi kucheza timu mbalimbali nje ya Afrika kama Heracles ya Uholanzi (1976-78), New York Eagles (1978) na kutimkia Austalia katika club ya Australian (1980) na mwaka 1981 alienda kucheza soka Dubai katika club ya Al Nasri iliyokuwa moja ya timu tishio katika Ligi Kuu ya Dubai na mwaka 1984 aliamua kurudi Tanzania na kustaafu rasmi kucheza soka.

Msimamo wa Beno Kakolanya Yanga ndio huu, katuma tena barua

Soma na hizi

Tupia Comments