Habari za Mastaa

Fat Joe aeleza sababu za kutotaka ukaribu na Tekashi 69

on

Inaelezwa kuwa mtu wa kwanza kumpa ushauri Rapper Tekashi 69 aachane na ukorofi ni Rapper Fat Joe ambapo alitumia podcast yake kufanya hivyo. Tekashi alihukumiwa kifungo cha miaka 4 jela kutokana na kosa la kumtumia kingono msichana wa miaka 13 mwaka 2015 pamoja na kujihusisha na uhalifu.

Katika kipindi cha Angie Martinez Show, Fat Joe amezungumza na kusema kuwa haitatokea tena yeye kuwa karibu na Tekashi 69 na wala hatosikiliza nyimbo zake. Kauli hii inakuja baada ya Tekashi   kutosikiliza ushauri wa Fat Joe na kuendeleza vitendo vya uhalifu mpaka kufikia hatua ya kupelekwa jela.

“Nilijua ni mtu mwema kwa sasa hivi hawezi kuwa rafiki yangu na haitotokea tena yeye kuwa karibu na mimi hata nikiingia kwenye viwanya vya kujivinjari sitoelewa  nikimkuta Dj anacheza ngoma ya Tekashi 69 “ >>>Fat Joe

VIDEO: TOFAUTI KATI YA MCHANA NA USIKU DARAJA LA NYERERE (KIGAMBONI)

Soma na hizi

Tupia Comments