Mwimbaji Chris Brown amekanusha taarifa zilizomchafua siku kadhaa zilizopita kuhusiana na tuhuma za ubakaji zilizokuwa zikimkabili baada ya mwanamke mmoja kudai kufanyiwa kitendo hicho katika hoteli ya Le Mandarin Oriental Ufaransa.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Chris Brown amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa yaliyozungumzwa ni uongo hayana ukweli wowote na aliongeza kwa kusema kuwa tuhuma hizo zimemfanya kumchafua na kumkosea heshima mbele ya familia yake pamoja na mtoto wake Royalty.
Huku taarifa nyingine zikiripotiwa kuwa Chris Brown ameachiwa huru kutoka kwenye mikono ya polisi nchini Ufaransa bila kufunguliwa shtaka lolote.
EXCLUSIVE: Dr Ipyana kaongelea M.40 zilizotumika kwenye Album yake ‘Hata hili litapita”