Habari za Mastaa

VIDEO: Filamu ya ‘Us’ ya Lupita Nyong’o yaweka rekodi kwenye mauzo ndani ya wiki

on

Mwigizaji kutokea nchini Kenya Lupita Nyong’o ameweka rekodi nyingine kwenye mauzo ya filamu mpya ya ‘Us’ baada ya kufanya vizuri kwenye filamu ya Black Panther iliyotoka February 2018.

Kupitia filamu hiyo mpya ya ‘Us’ ambayo Lupita amecheza kama muhusika mkuu (main character) imeweza kuingiza jumla ya dola za Kimarekani 70.2 milioni sawa na zaidi ya shilingi bilioni 165 za Kitanzania kwenye wiki yake ya kwanza ambapo ilitabiriwa kuingiza kiasi cha ($68 million) sawa na Tsh. bilioni 159.

Inaelezwa kuwa filamu ya “Us” ambayo imeongozwa na kuandika na Jordan Peele iliachiwa rasmi March 8, 2019 kwa mfumo wa trailer na ilitengenezwa kwa bajeti ya dola milioni 20 za Kimarekani sawa na zaidi ya bilioni 46 za Kitanzania, kutokana na mauzo hayo, filamu ya “Us” inatajwa kuwa filamu ya kutisha iliyouza zaidi duniani kwenye wiki ya kwanza kwa muda wote.

ULIPITWA NA USHINDI WA TAIFA STARS/ RUBY KUPATA MTOTO/ FLAVIANA NA RIHANNA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO.

Soma na hizi

Tupia Comments