Michezo

VIDEO: Hakuna siri siamini juju, Kagere anahitaji mpira tu kufunga

on

Simba SC Club leo walikutana na Azam FC katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania bara uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mchezo huo ulimalizika kwa Simba SC kupata ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 49.
Hii ni mechi ya tano kwa Simba SC msimu huu Meddie Kagere nae akiwa anaendeleza ukurasa mzuri wa ufungaji kwani kila mchezo wa Ligi Kuu ameshinda, baada ya mchezo tulimuuliza kocha wa Simba SC Patrick Aussems ni nini siri ya mafanikio yake?
“Kwanza nafikiri hakuna siri mimi siamini katika uchawi hivyo hakuna siri sisi tunafanya kazi kama timu hivyo hakuana siri, niliwaambia kabla ya mchezo hii itakuwa mechi ngumu kwa sababu Azam FC wana timu nzuri na wametuonesha leo nafikiri tulikuwa bora kuliko wao, kuhusu Kagere anahitaji mpira tu kufunga”>>>Aussems


AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments