Habari za Mastaa

“Rafiki zangu nimewahi kuwasimulia mkasa wangu wa Mbudya” -Haji Manara

on

Afisa wa habari wa timu ya Simba Haji Manara ni moja kati ya watu maarufu Tanzania walioguswa na kifo cha producer Pancho Latino kilichotokea October 9,2018 katika kisiwa cha Mbudya Dar Es Salaam.

Haji Manara ameelezea story yake ya kuwahi kunusurika kuzama katika kisiwa hicho za Mbudya enzi hizo bado mdogo na kusema kuwa alitoa shahada ya sala na ndipo alijikuta ufwekeni na tokea hapo maji anayoyafahamu ni ya kunywa na kuoga tu.

“Rafiki zangu wengi nishawahi kuwasimulia mkasa wangu na kisiwa cha Mbudya udogoni nikiwa na wazazi na ndugu zangu nilikaribia kuzama pale wakati nikiogelea nilifundishwa madrasa utotoni kabla ya kufa utoe Shahada Na nilishaisema kumaliza tu shahada ( لا إله الا ّالله محمد رسول الله )”

“Nikajikuta maji yamenisukuma ufukweni toka siku hiyo maji nayajua ya kunywa na kuoga bafuni tu kuogelea mwisho maji ya Ugoko
Yasemwa kifo cha kwenye maji na cha moto ni vifo vibaya zaidi na mwenzetu ametangulia mbele ya haki .Tumuombee Maghfira na cc Tujiombee Mwisho Mwema”

Mastaa wanavyomlilia Producer Pancho Latino

Soma na hizi

Tupia Comments