Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa ukuta wa mirerani na baadhi ya faida zake kuanza kuonekana moja kwa moja , kwa kushirikiana na chama cha wafanyabiashara wa madini nchini TAMIDA… Jopo la wanunuzi wakubwa wa Tanzanite duniani limetembelea eneo la machimbo ya migodi ya Tanzanite.
Shabaha ikiwa ni kujionea na kujiridhisha namna madini hayo yanavyo chimbwa na jitihada ambazo tayari zimefanyika katika udhibiti utoroshaji wa madini hayo, ambao kwa namna moja au nyingine ulikuwa ukiathiri bei ya madini hayo.
September 2017 wilayani Simanjiro mkoani manyara katika eneo la machimbo ya migodi ya madini ya Tanzanite Mirerani, Rais Dr John Magufuli alitoa agizo la kujengwa ukuta eneo lote la migodi hiyo na kuwa na mlango mmoja pekee ili kudhibiti ujichambaji holela na utoroshwaji wa madini ya Tanzanite.
Kwa sasa tayari Imeelezwa kuwa mapato ya serikali yameongezeka kutoka milioni 70 mpaka kufikia takribani Bilioni tatu kwa mwaka, Kwa upande wao wageni walio tembelea migodi hiyo kutoka nchini Marekani wameonesha kuridhishwa na hatua ya ujenzi wa ukuta na kuanza kuamini kuwa madini hayo yanapatikana Tanzania pekee.
VIDEO: Mpoki alivyomvunja mbavu Rais Mstaafu Kikwete