Wajumbe katika mkutano wa Uongozi wa Bara la Afrika wamezitaka nchi za Afrika kujenga mfumo imara wa ugavi wa thamani kwa kilimo kwasababu sekta hiyo inatoa fursa bora ya kuongezeka kwa biashara ndani ya Afrika.
Viongozi na washiriki wengine walibainisha kuwa Afrika ina ardhi ya kutosha kwa kilimo ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji na maendeleo ya bara hilo, ikishikilia zaidi ya nusu ya ardhi ya kilimo duniani na rasilimali kubwa za maji zenye uwezo wa kutosha kwa umwagiliaji.
Zaidi ya hayo, kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa bilioni 1.3 ambapo wengi wao (angalau asilimia 70) wanaishi vijijini na wanajishughulisha na kilimo kama shughuli yao kuu ya kiuchumi inaonekana kuwa ni jambo la kushangaza kwamba bara hilo bado linachangia asilimia 4 tu ya uzalishaji wa kilimo ulimwenguni pote, walibainisha.
Akizungumza katika Mkutano huo wa Uongozi wa Afrika (ALF) ambao ulianza hapo Alhamisi, Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete alibainisha kuwa sekta hiyo ilichangia sehemu kubwa ya Pato la Taifa na mapato ya fedha za kigeni kwa bara hilo na hivyo kutoa fursa ya kipekee kwa biashara ya ndani ya Afrika inayohitajika sana.
“Hakuna sekta inayowaajiri watu wengi kama kilimo, lakini bado haijafikia uwezo wake kamili, kwa hiyo kujadili jinsi ya kufungua uwezo wake ni jambo sahihi kufanya. Zaidi inahitajika kufanywa katika nchi za Afrika na kuunganisha na jinsi ya kuondoa umasikini, kuondoa upungufu wa chakula na njaa. Hii ni fursa kubwa kwa ushirikiano katika mnyororo wa biashara ya ndani ya Afrika,”alisema
Taasisi ya UONGOZI imeandaa Mkutano wa 7 wa ALF mwaka huu kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) kwa kauli mbiu “Kukuza biashara ndani ya Afrika ili kufungua uwezo wa kulimo barani Afrika.
“Kama Mwenyeji na Mlezi wa ALF, Dkt. Kikwete, alibainisha kwamba kilimo ni nguzo kuu ya watu wengi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na utinwa mgongo wa uchumi, hakuna mahali bora pa kuanza katika kipaumbele cha kuzingatia na uvumbuzi ikiwa bara linataka kuongeza biashara kati yao,” alisisitiza.
Alisema sekta hii muhimu haijafanikiwa kufanya kazi kikamilifu kwasababu ya vizuizi vingi vinavyozuia utumiaji kamili wa uwezo wake. Kwahivyo, kwa Jukwaa hili kujadili kufungua uwezo wa kilimo barani Afrika ni jambo sahihi kufanya.
Dkt. Kikwete alikiri kuwa juhudi zinafanywa na Serikali za Afrika kwa ajili ya wakulima wadogo wa Kiafrika na wadau wengine ili kubadilisha hali ya kilimo barani Afrika na kwamba tayari kuna maendeleo makubwa yaliyofikiwa na mafanikio mengi yamepatikana.
“Hatahivyo, kuna mengi zaidi yanahitajika kufanywa ili kilimo kiweze kuchangia kikamilifu katika ukuaji na maendeleo ya mataifa ya Afrika na ustawi na utajiri wa watu wa Afrika,” alisema.
“Mpaka sasa mambo yamekwenda vizuri lakini bado hayatoshi kama inavyothibitishwa na kiwango cha umasikini katika maeneo mengi ya vijijini ambap watu wetu wengi wanaishi na ripoti zisizoisha za watu kusumbuliwa na ukosefu wa chakula na njaa barani Afrika.” alisema
“Uwekezaji katika watu wetu hasa wakulima wadogo na vijana wetu; uwekezaji katika taasisi na miundombinu yetu ili kuhakikisha mazingira mazuri ya kufanya biashara yanahitajika; na zaidi ya yote kujitolea kwetu kuwekeza katika ajenda ya muda mrefu ya Afrika kuliko vipaumbele vya ndani vya muda mfupi.