Michezo

Juma Mgunda kuhusu Manula kutoitwa tena Taifa Stars

on

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Juma Mgunda amtolea ufafanuzi la swali la waandishi wengi kuhusiana na kutoitwa tena kwa Aishi Manula katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.

Juma Mgunda amewajibu wanaohoji kwa nini Manula anaendelea kukosekana katika kikosi cha Taifa Stars, mechi ya mwisho ya Aishi Manula kucheza Taifa Stars ilikuwa dhidi ya Kenya katika michezo ya AFCON 2019 iliyofanyika nchini Misri, CHAN dhidi ya Kenya mechi 2 ugenini, Burundi mechi 2, Rwanda, Sudan mechi 2.

“Sisi hatuchagui sura yake sababu sisi hatujikuposa sisi huku, tunamchagua mchezaji mtanzania mwenye uwezo wa kucheza kama vile Aishi alivyokuwa anachaguliwa nyuma kuna magolikipa walikuwa hawachaguliwi”>>> Juma Mgunda

“Kuchaguliwa kwa mchezaji mwingine kucheza badala yake ni suala la kawaida nae itafika wakati ataitwa tu kama Juma (Kaseja) amekaa nje ya timu miaka 6 leo kaitwa tena”>>>Juma Mgunda

TOP 5: Samatta anaondoka UEFA Champions League na rekodi hizi

Soma na hizi

Tupia Comments