Habari za Mastaa

Jumba la kifahari alilohamia Davido huko Banana Island nchini Nigeria

on

NI Headlines za msanii kutokea Nigeria Davido ambae anamiliki vichwa vya habari nchini Nigeria baada ya kuhamia Banana Island huko lagos nchini Nigeria.

Davido anasema aliondoka alipokuwa akiishi zamani na kuhamia Banana Island kutokana na matunda ya wimbo wake wa Falling , sasa mashabiki wanajiuliza Je atakuwa amenunua Jumba hilo ama atakuwa amepanga.

Kwanza nikujuze kidogo historia ya Banana Island ni kisiwa kidogo kilichotengenezwa  huko Ikoyi Lagos nchini Nigeria na kikamalizika mwaka 2000 ni kama Paradise ya matajiri na ndio waliojaa huko na wanapapenda kwasababu kuna amani, utulivu na vilevile ni mbali pia ndio jiji lenye watu wengi zaidi nchini Nigeria.

Jina la Banana limetokana na umbo lake la kitofauti sana na watu wanaoishi huko ni watu wenye fedha zao ndio maana Davido amehamia huko,  sasa maswali yanayoibuka  mitandaoni mashabiki wanahoji Je ni kwamba amenunua ama amepanga.Lakini kiukweli kwa mafanikio aliyoyapata msanii huyo sio jambo la acabou kumiliki jumba hili la kifahari.

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments