Waziri wa Nishati, January Makamba amesema kutokana na mipango ya Serikali, wanategema ifikapo mwezi Juni mwaka 2024 vijiji vyote Tanzania vitakuwa vimeunganishwa na umeme.
Waziri Makamba ameyasema hayo wakati wa maonyesho ya wiki ya Nishati akihojiwa na Clouds TV na kuongeza kuwa Serikali ina mipango inayozingatia utabiri wa hali itakavyokuwa mbeleni, lakini pia inaishirikisha zaidi sekta binafsi katika kuwekeza kwenye sekta ya nishati ili kuweza kufikia malengo kwa wakati.
Mbali na hilo Waziri wa Nishati, Makamba amesema kuwa >>“Tunachokifanya sasa hivi ni kuongeza vyanzo vingine na kupunguza utegemezi wa maji, ili kwanza kuondokana na ‘risk’ zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia kuwa na gridi ambayo ni imara zaidi” – Waziri Makamba.
Wizara ya Nishati inategemea kuwasilisha bungeni makadirio ya bajeti yake ya mwaka wa fedha 2023/2024 kuanzia siku ya Jumatano May 31 2023.