Habari za Mastaa

Kumbe Justin Bieber bado anampenda Selena Gomez, kazungumza haya kwenye jarida la Billboard! + (Pichaz).

on

Zikiwa zimebaki siku chache tu mpaka msanii wa muziki wa Pop kutoka Marekani, Justin Bieber aisogeze kwetu Album yake ya kwanza ndani ya miaka mitatu, Purpose, msanii huyo amepata shavu la kuonekana kwenye toleo jipya la jarida la Billboard la Marekani.

Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amezungumzia vitu vingi kwenye jarida hilo ikiwemo kuvuja kwa picha zake za utupu, mpenzi wake wa zamani Selena gomez na mtazamo wake kuhusu umaarufu wa wadogo zake Kim kardashian,  Kylie Jenner na Kendel Jenner.

BILLBOARD2

Kuhusiana na kuvuja kwa picha zake za utupu ambazo zilipigwa bila ridhaa yake mwenyewe, Justin Bieber ameliambia jarida la Billboard kuwa kitendo cha picha zile kupigwa na baba yake ilikuwa ni uvamizi wa maisha binafsi, japo baba ni baba…

>>> Ile picha kupigwa ilikuwa ni kitendo kinachoingilia maisha yangu binafsi. Niliona nimedhalilishwa kwa hali ya juu, lakini baba yangu aliniambia nisiichukulie serious. Badaae nikaona kama kichekesho tu… Nilikuwa naogopa, na hapo mwanzoni nilipoiona ilikuwa imeniziba kwa nyuma, nilisema Yesu wangu ni nini hiki” <<< Justin Bieber.

BILLBOARD4

Kuhusiana na Mpenzi wake wa zamani Selena Gomez, Justin Bieber amesema anajivunia kuona mafanikio yake makubwa kwa sasa, na amedai kuwa unapompenda mtu hata kitu kikija kati yenu upendo ulionao juu ya mtu huyo utabaki pale pale…

>>> “ Najivunia sana kumuona jinsi alivyokua mpaka kufikia hii leo… ukimpenda mtu kwa kiasi hiki hata kije nini kati yenu upendo mlionao kati yenu hauwezi kufa…” <<< Justin Bieber.

Hapa chini nimezisogeza kwako baadhi ya picha alizopiga Justin Bieber kwenye cover shoot ya jarida la Billboard.

BILLBOARD3

BILLBOARD5

BILLBOARD6

BILLBOARD7

BILLBOARD8

BILLBOARD9

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments