Habari za Mastaa

Justin Bieber anazisogeza zote 13 kutoka kwenye Album yake mpya ‘Purpose’ – (Videos)!

on

Miaka miwili iliyopita, December 2013 Beyonce Knowles aliachia Album yake iliyopewa jina BEYONCE kisiri siri, Album ambayo pia ilisindikizwa na suprise music videos ya kila single iliyokuwa inapatikana kwenye Album hiyo, na kwa muonekano wa mambo mwaka huu, Justin Bieber hajacheza mbali na  formula ya Beyonce!

BEEBA3

Baada ya kuachia Album yake ya nne iliyopewa jina Purpose, msanii wa muziki wa Pop kutoka Marekani, Justin Bieber ameamua kufuata nyao za Queen wa muziki wa Pop R&B, Beyonce Knowles kwa kuachia na yeye suprise videos 13 kutoka kwenye Album yake mpya siku ya jumamosi weekend iliyopita.

BEEBA

Japo kuna tofauti ndogo kati ya Justin na Beyonce Knowles, ujio wa Album mpya ya Justin ilikuwa tayari imeshapangwa kutoka wakati ujio wa Album ya Beyonce ya December 2013 ilikuwa ni ya kushtukiza huku kila kitu yani nyimbo na video viliachiwa kwa wakati mmoja wakati Justin Bieber aliamua kutoa video mmoja baada ya nyingine kila baada ya lisali moja siku ya jumamosi.

BEEBA2

Wakati Beyonce alionekana kwenye kila video aliyoitoa mwaka 2013, Justin Beiber anaonekana kwenye video mbili tu huku nyingine zote zinabebwa na dancers wake tofauti… video hizi zimepewa jina ‘Purpose: THE MOVEMENT.

BEEBA5

Hapa chini nimekusogezea zote 13 kutoka kwenye Album mpya ya Justin Bieber ‘Purpose’, feel free kuipitia moja baada ya nyingine mtu wangu.

  1. Justin Bieber – What Do You Mean?

2. Justin Bieber feat Halsey – The Feeling.

3. Justin Bieber, Skrillex & Diplo – Where Are U Now.

4. Justin Bieber – Company.

5. Justin Bieber feat Travis Scott -No Sense.

6. Justin Bieber – Purpose.

7. Justin Bieber – Love Yourself.

8. Justin Bieber – Life Is Worth Living.

9. Justin Bieber – Mark My Words.

10. Justin Bieber – I’ll Show You.

11. Justin Bieber  feat Big Sean – No Pressure.

12. Justin Bieber – Children.

13. Justin Bieber – Sorry.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments