Michezo

Juventus wapewa point za mezani

on

Club ya Juventus ya Ligi Kuu Italia (Serie A) leo imepewa ushindi wa magoli 3-0 na point 3 dhidi ya Napoli ambao walishindwa kufika uwanjani October 4.

Napoli ambao walishindwa kuwasili uwanjani sababu ya kutopewa ruhusa na mamlaka ya afya katika mji wa Naples kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona katika mji huo, wamepokonywa point moja kama sehemu ya adhabu pia.

Juventus licha ya kutambua mapema kuwa wageni wao Napoli hawatofika katika mchezo huo, waliwasili uwanjani na kufuata taratibu zote za mchezo ili kukwepa adhabu ambayo imewakumba Napoli.

 

Soma na hizi

Tupia Comments