Club ya Juventus ya Italia leo imeshinda rufaa yake ya kukatwa alama 15 za Ligi Kuu soka Italia kwa makosa ya udanganyifu katika vitabu vyake vya fedha tofauti na matakwa ya kisheria.
Chama cha soka Italia (FIGC) kilifanya uamuzi huo wa kuwakata alama 15 Juventus pamoja na kuwafungia miezi 24 aliyekuwa Rais wa Juventus Andrea Agnelli na Makamu wake Pavel Nedved miezi 8 baada ya kuwakuta na hatia ya makosa ya udanganyifu katika vitabu vya fedha na usajili.
Sasa Juventus wanashika nafasi ya tatu kutoka nafasi ya 7 baada ya alama zao 15 kurudishwa sasa wana alama 59, nyuma ya Napoli anayeongoza kwa 75 na Lazio anayeshika nafasi ya pili kwa alama 61 ila waendesha mashtaka wana nafasi ya kupinga rufaa hiyo ndani ya mwezi mmoja.