Habari za Mastaa

Jux aelezea jinsi alivyoandikiwa One More Night na Walter Chilambo

on

Sasa hivi kitu kipya kutoka kwa Jux ni audio na video ya One More Night. Jux akiongea na millardayo.com amesema kwamba ameamua kuimba ngoma ya mapenzi kwa idea ambayo hajawai kutumia hapo zamani. Akielezea kuhusu alichoimba kwenye wimbo huo alisema hivi, “Mimi nimekutana na msichana ninaye muimbia mara moja tu. Sasa baada ya hapo msichana hakutaka tena uhusiano na mimi, lakini mimi natamani tuendelea au itokee One More Night kama ile ya mwanzo”

Kama ulikua hujui ni kwamba wimbo huu Jux ameandikiwa na Walter Chilambo, “Walter ameandika wimbo huu na mimi nilitaka kufanya kitu cha tofauti kabisa, kama kawaida tumekuta beat na Walter alikua na idea ya kuandika wimbo wa aina hii. Kwasababu nimeandika sana ngoma zangu mimi mwenyewe, sasa hivi nilitaka kujaribu kitu kipya, so kuanzia uandishi hadi melody ni kazi ya Walter Chilambo”, alisema Jux

Video yenyewe ni hii hapa.

Tupia Comments