Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

AyoTV

VIDEO: Mtoto kaeleza baba yake alivyofariki uwanja wa Taifa akiishangilia Taifa Stars

on

Jumapili ya September 8 2019 ni siku ya majonzi kwa wapenzi wa soka kufuatia kutokea kifo cha shabiki wa soka mzee Christopher Rupia mwenye umri wa miaka 60, kifo cha mzee huyo kimetokea uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati wa mchezo wa kuwania kuingia makundi ya kufuzu kucheza Kombe la 2022 nchini Qatar.

Mtoto wa marehemu Mika Rupia ameeleza kuwa baba yake alikuwa sehemu ya watanzania waliokuwa wamejitokeza uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa Stars ikicheza dhidi ya Burundi lakini mzee huyo hakufanikiwa kumaliza kuangalia mchezo huo na kujikuta akipoteza maisha akiwa uwanjani.

Mzee Christopher amezikwa leo Mongolandege jijini Dar es Salaam na mazishi yake yakiwa yamehudhuriwa na watu mbalimbali wa soka akiwemo katibu mkuu wa TFF Wilfred Kidao, hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa Taifa Stars kupata ushindi wa penati 3-0, baada ya dakika 120 kumalizika wakiwa 1-1 (aggregate ikiwa 2-2), Unaweza kutazama video kamili ya mtoto wa marehemu akieleza baba alivyopoteza maisha.

EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE

Soma na hizi

Tupia Comments