Habari za Mastaa

Joh Makini ataja wasanii wa bongo anaowakubali kwenye muziki wa Hip Hop

on

March 31, 2017 kwenye XXL ya Clouds FM msanii  wa Bongo Fleva Joh Makini kutoka WEUSI ameelezea hisia zake kuhusu Rapa wa kike Rosa Ree pamoja na kolabo yake na msanii Davido kutoka Nigeria.

Joh amedai kuwa kwake Rosa Ree ni rapa namba moja kutokana na uwezo mkubwa wa kubadili style yake na akibainisha kuwa kama ataongeza juhudi atafanikiwa zaidi huku akiwataja wasinii wengine wa Hip Hop anaowakubali

>>>”Kwangu mimi Rosa Ree ni rapa namba moja, kama atakaza kwenye game japo ni binti namuona next level. Wengine ninaowakubali kwenye game ya Hip Hop Bongo yupo pia Motraa pamoja na washikaji wa OMG.” – Joh makini.

Mbali na hayo, Joh Makini amekataa kuizungumzia collabo yake na Davido akiwataka mashabiki wake kuisubira kwa kuwa alishaizungumzia sana.

Ulipitwa na alichosema Fid Q kuhusu Joh Makini. (+VIDEO)

Soma na hizi

Tupia Comments