Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), ameachiwa kwa dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Shilingi Milioni 10 baada ya kusomewa mashtaka matatu ya kutoa maneno ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mara baada ya kuachiwa Zitto alizungumza na vyombo vya habari nje ya Mahakama ambapo amesema anashukuru kwa mshikamano uliionyeshwa na Watanzania bila kujali vyama vyao na hali yao.
Amesema huo ni mchakato wa kawaida kwa wanasiasa kwani wamefungwa wakina Mwalimu na Nyerere, isiokuwa kikubwa anasikitika kutoshiriki Kongamano lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Tumeona watu na Ukasuku wa kueleza bila kujali hali harisi ya nchi yetu ilivyokuwa mbaya, naamini tutapata muda wa kufafanua ili kupata tafsiri mbadala kwa kile walichokifanya,”