Top Stories

Mahakama Kuu:Hatima Hukumu ya Mtoto wa Chacha Wangwe, Machi 27(+video)

on

Mahakama Kuu ya Tanzania inatarajia kutoka hukumu Machi 27, 2019 kuhusu rufaa ya  Mtoto wa Marehemu Chacha Wangwe ambae alikua Mbunge wa Tarime, Bob Chacha Wangwe akipinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutiwa hatiani kwa kuchapisha maneno 29 kwenye mtandao wa Facebook.

November 15, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuhukumu Bob kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela au kulipa faini ya Shilingi Milioni 5 baada ya kupatikana na hatia kwenye kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa FACEBOOK.

Hukumu hiyo ilisomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo alisema katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 6 na vielelezo 5 dhidi ya Bob ambae pia ni Mwanaharakati.

WAZIRI ASEMA MAFURIKO NI FURSA ” ISIONEKANE LAANA, TUTAPELEKA DODOMA”

Soma na hizi

Tupia Comments