Aliyekuwa Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli ametoa ambaye pia Mjumbe wa Taasisi ya kusimamia hifadhi mbalimbali Afrika (APN) amesema atamshawishi Mjukuu wa Malkia Elizabeth, Prince Harry ili atoe kipaumbele kwa hifadhi za Tanzania.
Lembeli amesema anatarajia kutoa ushawishi huo kwa Prince Harry kupitia mkutano wa siku mbili, ambao umeanza leo Novemba 13 na kuisha November 14, 2018 jijini London Uingereza ambao unawashirikisha wajumbe mbalimbali wa sekta ya utalii duniani.
Pia amesema katika mkutano huo pia watajadili namna bora ya kutumia pesa zinazochangwa na wadau mbalimbali kuimarisha uhifadhi duniani.
“Prince Harry, ni Rais wa Taasisi ya Afrika inayoshirikiana na
Serikali za Kiafrika kwa kuwa nimekuwa Mjumbe wa Bodi ya taasisi hii tangu mwaka 2008, nitaendelea kujitahidi kuishawishi duniani na Prince Harry mwenyewe atoe kipaumbele kwa hifadhi za Tanzania ili tuweze kufaidika na rasilimali zetu,” amesema.
Taasisi ya APN mpaka sasa inashirikiana na serikali za Malawi, Zambia, Msumbiji, Rwanda, Benin, Chad, Congo DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Gabon. Katika nchi hizo inaendesha kwa mkataba maalum na serikali hifadhi za taifa za nchi hizo ambazo zilikuwa zimekufa.
BAJAJI ILIYOBUNIWA TANZANIA BADO HAIJAREKEBISHWA ‘NIMEKATISHWA TAMAA’