AyoTV

VIDEO: Madiwani wasababisha Meya aahirishe kikao…kisa?

on

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire leo August 16, 2017 amelazimika kuahirisha kikao cha ndani cha kupokea taarifa za utekelezaji shughuli za Kata kwa robo ya nne 2016/17 baada ya Madiwani 19 kusema hawana imani naye.

Mmoja wa madiwani hao, Donata Gapi ambaye ni Diwani wa Mkuyuni, amesema madiwani walikwishakubaliana na kuweka saini za kutokuwa na imani na Mstahiki Meya ambapo walikuwa wanasubiri majibu ya hoja walizoziwasilisha katika azimio hilo.

Naye Mstahiki Meya ameeleza kushangazwa na Madiwani hao walioshindwa kuhoji mambo ambayo yameazimiwa kwenye vikao, kama suala la dampo la Buhongwa ambalo limejengwa kinyume na utaratibu badala ya kusema hawana imani naye.

Tazama kwenye hii video ina kila kitu!!!!

Kitu Waziri Nchemba ameagiza baada ya ajali ya moto wa Mbeya…PLAY KWENYE HII VIDEO KUTAZAMA!!!

Soma na hizi

Tupia Comments