Rajab Yattery ni kijana wa kitanzania ambae alihitimu masomo katika chuo cha Institute of Information Technology na kufanikiwa kupata Degree.
Rajab Yattery ambae anajulikana kwa jina la Dj K3 anasema mbali na kwamba aliamini angepata kazi mapema kutoka na ngazi ya Elimu aliyonayo lakini ilikuwa tofauti.
akizungumza na Millardayo.com anasema..>> “Baada ya kupata kuhitimu masomo yangu ya IT kiukweli maisha hayakuwa rahisi hususani hizi ofisi zetu wanatabia ya kumuweka mtu benchi zaidi ya mwaka hata miaka miwili pale mtu anapoenda kuomba kazi kwahiyo sikufanikiwa kupata kazi kabisa kwa kile nilichokisomea”- DJ K3
“Basi nikakubaliana na matokeo huku nikimuomba Mungu, mahali ambapo nilipokuwa naishi nilikuwa nakaa na rafiki yangu ambae yeye alikuwa ni mchezeaji wa Santuli yaani ni Deejay“- DJ K3
“Maisha yakawa yanaenda huku nasubiria majibu kutoka katika zile ofisi nilizopeleka CV zangu huku nikijifunza kuchezea Santuli za U DJ nyumbani”- DJ K3
“Kiukweli namshukuru Mungu na wala sikukata tamaa niliweza kuelewa na jamaa yule ambae nilikuwa nikiishi nae alinipeleka kwa Carlos ambae ni mmiliki wa Samaki Samaki kisha nikapata kazi yangu ya kwanza ya kuzicheza nyimbo tofauti tofauti kwa muda wa masaa matano”– Dj K3
“Mrejesho wa wadau mbalimbali ulikuwa ni mzuri sana kwani najua nini nafanya pia kwasababu nilikuwa napenda sana muziki”– Dj K3
“Basi maisha yakaenda watu wakawa wanapenda muziki unaochezwa pale wakawa wanajaa Samaki Samaki enzi hizo ilikuwa ni balaa sana”- Dj K3
“Safari yangu haikuishia tu Samaki Samaki bali baada ya mkataba wangu kuisha mahali hapo niliamua kutafuta pengine ili kuendelea kujitafutia riziki”- Dj K3
“Wakati naendelea kutafuta kazi mahali pengine nikawa nakodisha santuli ili zinapotokea zile private party ambazo mteja anakuwa na sherehe fulani yenye uhitaji wa DJ basi ni makubaliano kuwa napiga muziki masaa kadhaa na malipo yanafanyika hivyo ndio ilikuwa sheria yangu”- DJ K3
“Basi kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo Mungu anabariki Mikono ya kazi yangu, nikaja kupata nafasi ya kuwa miongoni mwa Ma DJ watakaotoa burudani katika Tamasha la Nyamachoma Festival iliyofanyika katika viwanja vya chuo cha UDSM kiukweli sitosahau lile shangwe kwani ilikuwa ndio mara ya kwanza kuburudisha Maelfu waliofika katika ule uwanja ilikuwa balaa sana” – DJ K3
“Maisha ni safari ndefu sana kuna mengi utakutana nayo ni mazuri na mengine sio mazuri ila ni kumshukuru Mungu tu kwani hakuna jitihada zisizokuwa na mafanikio na hatimae leo nimeingia kwenye list ya Ma DJ wakubwa wenye kuaminiwa katika suala la utoaji wa burudani”- DJ K3
“Kwasasa kituo changu cha kutoa burudani ni Elements Bar Masaki kuanzia Alhamisi niko pale na Elements nimedumu nao takribani miaka 17 mpaka sasa kwahiyo ni kama Mama kwangu naheshimu sheria zao na wakati wanaponihitaji”- DJ K3
“Kufanya kazi Elements sio kwamba ndio siruhusiwi mahali pengine kufanya hapana kama Mteja wa nje anaponihitaji kuna maelewano tu, mimi nafanya kazi popote pale hata nje ya Tanzania”- Dj K3
“Mwisho ningependa kumalizia kwa kusema kwa nilipotoka mpaka hapa niliposasa ni kwamba Elimu tuwe nayo ila tuzingatie kipaji ni muhimu zaidi na zaidi pia leo Usiku nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa hivyo nawakaribisha wote mjumuike nami” – Dj K3