Zipo sehemu nyingi ambazo huwa na taratibu zake na kufuatwa ni lazima…moja ya sehemu hizo ni Mjimkongwe uliopo Zanzibar ambako sio kila gari, kila siku linaweza kuingia katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud amesema katika eneo la Mji Mkongwe kuna idadi maalumu ya magari yanayoruhusiwa kuingia kwa siku na si kila gari linaruhusiwa huku pia kukiwa na wakati maalumu wa magari kuingia.
>>>”Katika Mji Mkongwe kuna Traffic Master Plan ambapo kuna magari yenye tani maalumu ambayo hayazidi Tani mbili ambayo yanapaswa kuingi. Pia kwa mujibu wa mpango huo wa usimamizi wa magari yanayoingia Mji Mkongwe kuna idadi maalumu kwa siku. Sio kila gari, kila siku, kila wakati linaweza kuingia katika eneo hili.”