AyoTV

VIDEO: Humphrey Polepole baada ya kukutana na Rais Magufuli

on

Leo December 20 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi watatu wa CCM aliowateua hivi karibuni kujaza nafasi wazi katika safu ya uongozi wa chama ngazi ya taifa.

Viongozi hao ni Naibu Katibu Mkuu Bara Rodrick Mpogolo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Bw. Humphrey Polepole na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Siasa na Mambo ya Nje Kanali Mstaafu Ngemela Eslom Lubinga.

Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole amesema lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kumweleza Mwenyekiti wa CCM fikra na mipango ya awali na namna walivyojipanga kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama, kusimamia na kutekeleza ajenda ya mageuzi ndani ya chama ambayo msingi wake ni kuirejesha CCM kwa watu.

Rais ametuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba msimamo wa kufanya mageuzi kwenye Chama Cha Mapinduzi, kukirudisha kwenye misingi ambayo chama hiki kilianzishwa, yaani chama cha wanyonge na chama ambacho kinajinasibu na shida za watu, unatekelezwa’;-Polepole 

‘Ametuambia tukafanye kazi kwa bidii, Watanzania wana matumaini makubwa sana na Chama Cha Mapinduzi na sisi tumemhakikisha kwenda kuchapa kazi ili dhamira ya kujenga Tanzania mpya iweze kuakisiwa na kuletwa na CCM Mpya’;Polepole

VIDEO: ‘Kwanini mpaka sasa kuna kesi 1 tu Mahakama ya Mafisadi’ – Dr. Mwakyembe, Bonyeza play hapa chini kutazama

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments