Michezo

Cristiano Ronaldo anaendelea kudhiirisha ubora wake kwa kupindua matokeo

on

Usiku wa March 12 2019 Juventus walikuwa nyumbani kwao Turin kuikaribisha Atletico Madrid katika mchezo wao wa marudiano wa hatua ya 16 bora wa UEFA Champions League msimu wa 2018/2019, Juventus walikuwa wanaingia kucheza mchezo huo wakiwa nyuma kwa magoli 2-0 waliyofungwa katika mchezo wa kwanza.

Mpenzi wa Cristiano Ronaldo anayejulikana kwa jina la Georgina Rodriguez akilia baada ya Ronaldo kufunga hat-trick.

Hivyo kunusuru maisha yao katika michuano hiyo walikuwa wanahitajika kupata ushindi wa kuanzia mabao matatu na kuendelea, hata hivyo licha ya hofu kwa mashabiki wa Juventus kuwa kubwa kuwa wanaweza kulazimishwa sare kutoka Atletico Madrid kutokana na asili ya timu hiyo kuwa na safu nzuri ya ulinzi.

Wameshindwa kuhimili presha ya Cristiano Ronaldo wa Juventus na kujikuta akiingia wavuni mara tatu kwa kufunga hat-trick, Ronaldo aliifungia Juventus goli la kwanza dakika ya 27, 49 na 86 kwa mkwaju wa penati na kuindoka Atletico kwa kipingo cha magoli 3-0 (Agg 3-2), hivyo ni wazi Juventus imekata tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke 

Soma na hizi

Tupia Comments