Michezo

Baada ya kudaiwa kumalizana na Pep Guardiola, Juventus wamepiga hodi tena Real Madrid

on

Wakati kukiwa na uvumi mkubwa katika vyanzo mbalimbali vya habari za michezo vya Ulaya kuwa kocha wa sasa wa Man City Pep Guardiola mwisho wa msimu atahamia Juventus na tayari wamefikia makubaliano na club hiyo kwa kipindi cha miaka minne mara baada ya msimu huu kumalizika.

Inaonesha kuwa Juventus wameamua kuboresha kikosi chao kwa kiwango kikubwa na sasa wamerudi tena kuibomoa Real Madrid, baada ya kufanikisha kumuondoa Cristiano Ronaldo katika club ya Real Madrid na kumpeleka Turin, sasa wanamtaka wamchuku Marcelo kutoka club hiyo.

Kama Marcelo ataondoka Real Madrid na kujiunga na Juventus kama inavyoripotiwa atakuwa anaihama club hiyo baada ya kudumu nayo kwa miaka 12 toka 2007 alipojiunga nayo akitokea nchini kwao Brazil katika club ya Fluminense aliyoanza kuichezea tokea timu za vijana 2002 akiwa na umri wa miaka 14.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments