Michezo

Mourinho sasa inaripotiwa anaelekea Ufaransa baada ya dili za Hispania na England kudunda

on

Baada ya Zidane kutangazwa kuwa ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitatu na kumrithi Santiago Solari, taarifa hizo ziliondoa uwezekano wa Jose Mourinho kurudi kuifundisha tena Real Madrid kama ilivyokuwa inahusishwa hivi karibuni.

Mourinho ambaye amewahi kuifundisha Real Madrid 2010 amekosa nafasi hiyo na sasa uongozi wa Real Madrid umempa mkataba Zidane, inaelezwa kuwa kwa sasa Mourinho toka afukuzwe kazi Man United December 2018 kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu, amekosa timu England na Hispania alikokuwa anapewa nafasi.

Hata hivyo imeripotiwa kuwa Jose Mourinho ameanza kupewa nafasi ya kuifundisha timu ya PSG kwa siku za usoni, inaelezwa kuwa Mourinho anaweza akawa na nafasi ya kuifundisha PSG ambayo ipo chini ya kocha Tuchel ila kuna uwezekano wa kibarua chake kikaota nyasi na kuzibwa na Jose Mourinho ambaye hana timu toka December 2018 alivyofukuzwa na Man United.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

 

Soma na hizi

Tupia Comments