Michezo

Sir Alex Ferguson amefungiwa kwenda uwanjani kuangalia game za Man United

on

Kutoka mtandao wa The Sun wa England imeripotiwa kuwa kocha mkuu mstaafu wa club ya Man United Sir Alex Ferguson amekatazwa na madaktari kwenda uwanjani kuhudhuria game za Man United ili kuupa mwili wake nafasi ya kutosha kupumzika.

Taarifa hizo zimekuja kufuatia Ferguson kuonekana uwanjani na madaktari wake kupitia TV ndipo walipofuatilia wakagundua kuwa Ferguson alihudhuria game tatu mfululizo za Man United, ikiwemo game ya kusafiri iliyochezwa nyumbani kwa Southampton, safari ambayo ni mbali kwa afya yake ya sasa kumudu kusafiri.

Ferguson mwenye umri wa miaka 76 alikuwa sehemu ya watu walioshuhudia game ya Man United dhidi ya Fulham katika uwanja wa Old Trafford na kumalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 4-1, sare ya 2-2 dhidi ya Southampton na game dhidi ya Young Boys hivyo anapaswa apumzike asihudhurie mfululizo uwanjani kwa faida ya afya yake.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Ferguson ambaye aliifundisha Man United kama kocha mkuu kwa miaka 27 kuanzia mwaka 1986 hadi 2013, aliwahi kulazwa na kufanyiwa upasuaji katika ubongo wake mwezi May 2018, upasuaji ambao inaaminika ni hatari zaidi na mtu anaweza kupoteza maisha hivyo kwa afya yake atakiwi kuwa busy sana.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments