AyoTV

EXCLUSIVE: Ajib kamtaja aliyemuomba ushauri kuhama Simba kwenda Yanga

on

Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu ni moja kati ya wachezaji ambao uhamisho wao wa kutoka Simba SC kujiunga na Yanga ulichukua headlines sana kutokana na mchezaji huyo wengi hawakudhania kama anaweza akaihama Simba na kwenda Yanga.

Ajib ni zao la Simba ambapo ni miongoni mwa wachezaji wachache waliowahi kupandishwa na Simba kutoka team B na kufanikiwa kufanya vizuri, hivyo Amplifaya imemnasa katika exclusive interview na kumuuliza hivi ni nani alimuomba ushauri mwaka 2017 alipokuwa anaamua kujiunga na Yanga na kuikacha Simba SC.

“Kwenye hilo mimi mshauri wangu mkubwa ni mama yangu mzazi, kwa hiyo mimi nikiongea na mama angu mzazi akiridhia kila kitu basi mimi nafanya, mimi na mama yangu tunavyoishi kama mtu na rafiki yake hivyo ilikuwa kama tunazungumza tu kawaida sio kama watu wanavyoichukulia sijui nimpigie simu mama bwana kuna kitu kibwa hapana yani ilikuwa kawaida tu hivi tunazungumza”>>>Ajib

Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF

Soma na hizi

Tupia Comments