Baada ya mchezo wake wa kwanza dhidi ya Liverpool na KRC Genk kuchezwa katika uwanja wa Luminus nchini Ubelgiji, huku mtanzania Mbwana Samatta akifunga goli na kukataliwa dhidi ya Liverpool.
Usiku wa November 5 2019 kiu ya Tanzania ilikatwa rasmi na Mbwana Samatta ya kuona anafunga goli dhidi ya Liverpool, ili aweke rekodi ya kuwa mtanzania pekee wa kwanza kuwahi kuwafunga Liverpool.
Samatta akiwa na club yake ya KRC Genk alifanikiwa kufunga goli la kuisawazishia Genk dakika ya 41 kwa kichwa, hiyo ni baada ya Wijnaldum kuwafungia Liverpool goli la kuongoza dakika ya 14, Alex Chamberlain ndio aliweka msumari wa ushindi kwa Liverpool dakika ya 52 na kuufanya mchezo kumalizika 2-1.
Samatta sasa anaweka rekodi isiyovunjwa Anfield ya kuwa mtanzania wa kwanza kufunga goli Anfield achilia mbali rekodi aliyoiweka dhidi ya RB Leipzag ya kuwa mtanzania wa kwanza kufunga goli UEFA Champions League, Genk sasa inaondolewa rasmi katika michuano hiyo kwa kuwa na point moja hata wakishinda michezo yao miwili iliyobaki hawezi kumaliza nafasi ya pili.