Mix

Ni kweli viongozi wa serikali hawatapokelewa kwenye msiba wa Kabwe? ukweli upo hapa

on

Familia ya aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe leo May 22 2016 imeamua kutoa tamko au taarifa rasmi kwa vyombo vya habari kuwa, habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii sio za kweli kuwa familia haitopokea viongozi wa serikali katika shughuli za mazishi ya Wilson Kabwe.

Taarifa ya familia inaeleza kuwa Zawadi Machuve sio msemaji wa familia kauli yake iliyonukuliwa na vyombo vya habari ikieleza kuwa ‘sisi hatukaribishi viongozi, huu ni msimamo wa familia kama wao watafanya utaratibu wao sawa, lakini hatuko kwa ajili ya viongozi”

Kauli hiyo iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari sio ya kweli na wala sio kauli ya familia, kiukweli familia ya marehemu Wilson Kabwe inatambua, ina thamini mchango wa serikali katika kusaidia huduma za matibabu na kugharamia huduma za mazishi.

IMG-20160522-WA0024

ULIIKOSA HII YA OMBAOMBA WABISHI KUKAMATWA DA ES SALAAM? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments