Michezo

Kabla ya kupambana na Simba SC Jan 19, Alliance FC imerudi kwa jamii

on

Club ya Alliance FC ya jijini Mwanza ikiwa ni siku moja imesalia kabla ya kuikaribisha Simba SC katika uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania, leo wametembelea kituo cha watoto yatima na kutoa msaada kama sehemu ya kurudisha kwa jamii.

Kituo walichotembelea Allance FC kijulikanacho kama Watoto Afrika kilichopo Busweru jijini Mwanza.

 

Emirate Aluminiumco Ltd wanaouza bidhaa bora za Aluminium nchini waliongozana na viongozi pamoja na wachezaji wa Alliance FC.
katka kituo hicho cha watoto yatima chenye watoto 75 , wenye umri kati ya miaka minne hadi 20.

VIDEO: KABLA YA KUPAMBANA NA SIMBA SC JAN 19, ALLIANCE FC IMERUDI KWA JAMII

Soma na hizi

Tupia Comments