Ad
Ad

Michezo

Hii ndio Top 5 ya wachezaji wanaoongoza kwa kuoneshwa kadi nyingi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

on

Bado michezo nane hatua ya makundi imalizike, baada ya December 8 kuchezwa michezo nane lakini Usiku wa Jumatano ya December 9 ndio siku ambayo jumla ya timu 32 zitakuwa zimemaliza michezo yake ya hatua ya Makundi na kuweza kufahamu ni timu zipi zimeweza kutinga hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2015/2016.

Mtu wangu wa nguvu tukiwa bado tunasubiri hatua ya Makundi imalizike kwa michezo nane ya December 9 kuchezwa naomba nikusogezee Top 5 ya wachezaji soka wanaoongoza kwa kuoneshwa kadi nyingi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya toka kuanzishwa kwake.

5- Gennaro Gattuso anatajwa kuwa katika list ya wachezaji wenye hasira ila hasira zake zimemfanya aingie katika rekodi ya wachezaji wanaoongoza kwa kuoneshwa kadi nyingi, Gennaro Gattuso anatajwa kuoneshwa jumla ya kadi 23, kadi ambazo alizipata akiwa katika klabu ya Rangers na AC Milan.

Gattuso

Gennaro Gattuso

4- Carles Puyol ni miongoni mwa mabeki wa kati wachache wenye uwezo wa kumudu nafasi zao uwanjani kwa kufasaha, lakini katika suala la kuoneshwa kadi na marefa yeye ameoneshwa jumla ya kadi 25 katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya, kadi ambazo ameoneshwa akiwa na klabu ya FC Barcelona.

Carles-Puyol-g

Carles Puyol

3- Licha ya kuwa mshikaji wake Pepe hayupo katika hii list Sergio Ramos anamuwakilisha staa huyo kwa kuoneshwa jumla ya kadi 26 akiwa katika vilabu vya Sevilla na Real Madrid.

Sergio-Ramos6

Sergio Ramos

2- Xabi Alonso ni kiungo wa kimataifa wa Hispania ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani, Alonso yupo nafasi ya pili katika list ya wachezaji walioneshwa kadi nyingi zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Alonso ameoneshwa jumla ya kadi 27, kadi ambazo amezipata akiwa katika vilabu vya Real Sociedad, Liverpool, Real Madrid na sasa FC Bayern Munich.

Xabi-Alonso

Alonso

1- Paul Scholes kiungo wa zamani wa Man United ambaye kwa sasa amestaafu soka, licha ya kuwa amestaafu soka Paul Scholes rekodi yake ya kuoneshwa kadi nyingi bado haijavunjwa, kwani ameoneshwa jumla ya kadi 32 akiwa katika klabu ya Man United, lakini Scholes ndio mchezaji pekee ambaye anaongoza kwa tofauti kubwa kutoka mtu anayemfuatia kwani anapishana na Alonso kwa tofauti ya kadi 5.

Scholes1

Scholes

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments