Michezo

Matokeo ya mechi za July 26 na ratiba ya Robo fainali Kagame Cup 2015

on

kombeHatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Kagame imemalizika July 26 kwa timu tano kuaga mashindano hayo na timu nane kusonga katika hatua ya robo fainali itakayoanza siku ya Jumanne July 28… Timu zilizo tolewa mashindanoni kwa uchache wa point zao ni pamoja na Heegan FC ya Somalia Telecom ya Djbout na Adama City ya Ethiopia.

Azam-vs-KCCA-1Hatua ya makundi imemalizika kwa michezo miwili ya kundi A kupigwa katika Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya Gor Mahia ya Kenya dhidi ya Telecom ya Djbout mchezo amabao umemalizika kwa Gor Mahia kushinda kwa jumla ya goli 3-1.

image4Mchezo wa pili uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jioni ya July 26 ni Dar Es Young African dhidi ya Al Khartoum ya Sudan mchezo uliomalizika kwa bao pekee la Ammissi Tambwe dakika ya 30 ya mchezo na kuiwezesha Yanga kushika nafasi ya pili ya Kundi A.

timthumbKwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo Yanga sasa itakutana na mshindi Kundi C ambaye ni Azam FC July 29 katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, michezo mingine ni APR ya Rwanda itacheza na Al Khartoum ya Sudan, Gor Mahia ya Kenya itacheza na Best looser  July 28 na July 29 Alshandy ya Sudan na KCC FC ya Uganda.

MMGM0029Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments