Top Stories

KAGERA: Aliembaka mbuzi akamatwa

on

Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia, Emmanuel Zakaria Muhangaza (38) mkazi wa Lusahunga kwa kosa la kumbaka mbuzi mali ya Jacob Nyawenda.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Awadhi Jumaa amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Oktoba 24, Mwaka huu katika Kijiji cha Lusahunga wilayani Biharamulo ambapo mtuhumiwa huyo alikutwa na mbuzi akiwa marishoni kisha kumchukua na kumpeleka kichakani na kuanza kumbaka.

Amesema wakati mtuhumiwa huyo akiendelea na tukio hilo alipita mke wa jirani yake na mlalamikaji na kumkuta ambapo alitoa taarifa kwa wananchi wengine na mtuhumiwa aliwekwa chini ya ulinzi.

Kwa mujibu wa Kamanda Jumaa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za mwili “Mpaka sasa jeshi la polisi tunafanya utaratibu wa kumpima Afya ya akili ili tujue nini kinacho msumbua”

 

Soma na hizi

Tupia Comments