Mix

Kagera wa Simba aungana na Sibomana na Kaseke wa Yanga kwenye mchongo wa jero

on

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania leo imeingia kwenye ushirikiano na SportPesa Tanzania kwa kuzindua promosheni kabambe ambapo wateja watajishindia zawadi wanapobashiri mara baada ya kuweka pesa kwenye akaunti ya SportPesa kupitia Tigo Pesa.

Kupitia faidika na jero, wateja wataweza kujishindia zawadi aina ya smartphone kila siku wakati kwenye droo ya mwisho mteja mmoja atajishindia gari mpya Renault Kwid kwa kubashiri kuanzia kiasi cha Tshs 500 tu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema “Kupitia vyombo vya habari tutatangaza washindi wa kila wiki na atakabidhiwa zawadi yake bila gharama yoyote, Mteja atatakiwa kujisajili, kuweka fedha kwenye akaunti ya SportPesa kupitia mtandao wa tigo, kucheza na SportPesa ili ashinde’.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano Tigo Tanzania Woinde Shisael alisema, ‘Hii ni fursa nyingine kwa Tigo kuwazawadia wateja kupitia promosheni hii imekuwa ikizindua bidhaa na huduma zenye ubunifu wa hali ya juu na zinazokidhi matakwa ya wateja wetu.

‘Tunaelewa ni njisi gani wateja wetu wanapenda michezo na ni sehemu ya maisha. Kwa kupitia ushirikiano wetu huu na SportPesa, tunawapa wateja wetu fursa ya kujishindia zawadi kwa kubashiri na kuweka pesa kupitia Tigo Pesa’.

VIDEO: Moja kati ya magoli ya marehemu Jeba, hili liliwaumiza wana-Simba 2016

Soma na hizi

Tupia Comments