Michezo

Kagere kapigana na Kocha Sven?, Manara atoa tamko (+Audio)

on

Uongozi wa Klabu ya Simba SC umekanusha taarifa zilizoandikwa na kuripotiwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na vyombo vya Habari kuwa mshambuliaji wao Meddie Kagere amepigana na Kocha wake Sven Vandenbroeck.

Taarifa zilizotolewa kwenye mitandao ya kijami na baadhi ya vyombo vya habari, zimeeleza kuwa wawili hao walipigana wakiwa mazoezini Mjini Mbeya baada ya kuwasili wakitokea Arusha kupitia DSM.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC, Haji Sunday Manara amesema taarifa hizo sio za kweli, kwani zina lengo la kuvuruga amani ndani ya kikosi chao ambacho kipo tayari kuanza kutetea taji la Tanzania Bara mwishoni mwa juma hili dhidi ya Ihefu FC.

Soma na hizi

Tupia Comments