Usiku wa April 30, 2017 ziliripotiwa taarifa za tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera na kusababisha hofu na taharuki kwa wananchi ambao walilala nje ya makazi yao.
Ayo TV na millardayo.com imezungumza na Meya wa Manispaa ya Bukoba Chief Kalumna ambaye ameelezea hali ya wananchi ilivyo wakati huu hasa juu ya miundombinu.
“Wale ambao wanafikiri kwamba, kwa Mkoa wa Kagera hali imerudi katika hali ya kawaida kufuatia madhara yaliyotokana na tetemeko la ardhi mwaka jana, huo sio ukweli kabisa hata Kata yangu ya Kahororo wananchi bado wanalala nje.
“Lakini mimi as Meya ninaendelea kuhoji swali la namna hiyo kwamba ipo michango mbalimbali ambayo ilitolewa na mataifa mbalimbali labda Ofisi ya Waziri Mkuu inabidi ifike wakati waeleze walipata Shillingi ngapi, walitumia Shilingi ngapi kwa wananchi na wananchi wapi maana yawezekana tetemeko likatokea Kagera na michango ikachangwa ikaenda sehemu nyingine.” – Chief Kalumna.
Nimekuwekea full video, bonyeza play kutazama…
EXCLUSIVE: Mashuhuda wasimulia tetemeko lilivyotokea Kagera usiku wa kuamkia leo. Bonyeza play kutazama…