Ni Staa kutokea Bongo Movies, Kajala Masanja ambae leo Julai 15 ndio siku ambayo aliiandika katika maisha yake baada ya kupata mtoto wa kike ambae anafahamu kwa jina la Paula.
Akizungumza na millardayo.com ametumia nafasi huu kumtumia Ujumbe mwanae mpendwa Paula na ikiwa kama sehemu ya kumtakia baraka tele katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa siku ya leo….‘Kwako dada Pau, mtoto wangu wa pekee maisha yatakuwa na misukosuko, majaribu na tabu tele. Ila hakikisha tabasamu lako na furaha yako inakuwepo na wewe popote uendapo.
‘Nataka tu ufahamu wewe ni kitu changu cha thamani cha pekee nilichowahi kuwa nacho hapa duniani. Daima nilikuwepo, nipo na nitaendelea kuwepo kwenye maisha yako kukulinda na kukupigania na kila baya. Nakutakia heri ya sikukuu yako ya kuzaliwa my dear daughter. Mungu pekee ndiye wa kukulinda na kukubariki, Nakupenda zaidi ya neno kupenda’- Mwigizaji Kajala
Kwa Mujibu wa Kajala anasema Mwanae leo Julai 15 anatimiza miaka 21.
Millardayo.com & Ayo TV inamtakia Happy Birthday Paula ukawe na umri mrefu na wenye kutimiza hitaji la moyo wako.