Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini. Moja ya stori iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo June 14 2016, ni hii kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Kamati ya Bunge yamhoji Naibu Spika‘.
#MTANZANIA Kamati ya Bunge yamhoji Naibu Spika kuhusu maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kumwondoa pic.twitter.com/SEfBILyCJS
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
Gazeti hilo limeripoti kuwa kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge imemwita Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kujieleza mbele yake kuhusu maombi yaliyowasilishwa na mbunge wa Simanjiro, James ole Millya (CHADEMA) kutaka kumwondoa madarakani.
Taarifa zilizopatikana baadhi ya wabunge Dodoma jana na kuripotiwa na gazeti la Mtanzania zilidai kamati hiyo tayari imemuhoji Dk. Tulia kuhusiana na suala hilo, habari zinasema Dk. Tulia alihojiwa na kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake George Mkuchika ambayo endapo itaridhika kwa mujibu wa kanuni hoja hiyo itawasilishwa bungeni kwa ajili ya uamuzi wa bunge .
Alipoulizwa kuhusu lini kamati hiyo itakaa na kumhoji Dk Tulia mwenyekiti wa kamati hiyo George Mkuchika alisema haruhusiwi kuzungumzia shughuli za kamati hiyo kwa vyombo vya habari.
>>>‘kamati yetu inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, haturuhusiwi kusema nani kaitwa au kaandikiwa barua subirini kazi yetu inapokuwa tayari tunaiwasilisha bungeni‘
#NIPASHE Wabunge wapinga ongezeko la ushuru kwenye mitumba kwa kuwa utaua soko la wamachinga na kuongeza uhalifu pic.twitter.com/XcM7rHnk1A
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#MWANANCHI Zitto ahojiwa na Polisi kuhusu tukio la kusitishwa kwa kongamano lililolenga kujadili bajeti ya serikali pic.twitter.com/sBGId2KuYG
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#MWANANCHI Madereva wa UDART wamegoma wanataka kulipwa sh. 800,000 wakipinga mshahara wa sh.400,000 kwa mwezi pic.twitter.com/ycHki8I2re
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#MWANANCHI Waziri Nchemba awataka wafanyabiashara dawa za kulevya kuacha kwani Serikali haiwezi kuweka vijana rehani pic.twitter.com/ceyBHsmVVc
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#NIPASHE Baada ya CUF kutangaza azma ya kufanya uchaguzi Lipumba ameandika barua kuomba kurejea katika nafasi yake pic.twitter.com/acvR8VzCKy
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#MAJIRA Serikali imewataka askari kutimiza wajibu wa kupiga saluti kwa viongozi walioainishwa kwa mujibu wa sheria pic.twitter.com/N0R7Rk4LmA
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#MAJIRA Operesheni ya kukusanya kodi ya mabango, leseni za biashara, majengo Ilala yaingiza bil 1 kwa siku sita pic.twitter.com/SJWPviTtND
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#MTANZANIA Joshua Nassari na madiwani wanne Meru kizimbani Arusha kwa tuhuma za kuharibu mali kwa makusudi pic.twitter.com/PXLNx8p6Dt
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#NIPASHE Gaidi aliyepanga shambulio klabu ya mashoga aliwapigia simu polisi na kula kiapo cha utii kwa Islamic State pic.twitter.com/XLtliREQIZ
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#NIPASHE Wabunge wameendelea kuililia serikali isitishe mpango wa kukata kodi ktk kiinua mgongo wanachopata pic.twitter.com/voNvo6KCOE
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
#MWANANCHI Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mongella asema wamebaini kuwepo kwa vikundi vya kukodi vya uhalifu na mauaji ya watu pic.twitter.com/ZE2QmRDiGH
— millardayo (@millardayo) June 14, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JUNE 14 2014? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE