fB insta twitter

‘Kamati ya Bunge yamhoji Naibu Spika, Tulia Ackson’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini. Moja ya stori iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo June 14 2016, ni hii kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Kamati ya Bunge yamhoji Naibu Spika‘.

Gazeti hilo limeripoti kuwa kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge imemwita Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kujieleza mbele yake kuhusu maombi yaliyowasilishwa na mbunge wa Simanjiro, James ole Millya (CHADEMA) kutaka kumwondoa madarakani.

Taarifa zilizopatikana baadhi ya wabunge Dodoma jana na kuripotiwa na gazeti la Mtanzania zilidai kamati hiyo tayari imemuhoji Dk. Tulia kuhusiana na suala hilo, habari zinasema Dk. Tulia alihojiwa na kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake George Mkuchika ambayo endapo itaridhika kwa mujibu wa kanuni hoja hiyo itawasilishwa bungeni kwa ajili ya uamuzi wa bunge .

Alipoulizwa kuhusu lini kamati hiyo itakaa na kumhoji Dk Tulia mwenyekiti wa kamati hiyo George Mkuchika alisema haruhusiwi kuzungumzia shughuli za kamati hiyo kwa vyombo vya habari.

>>>kamati yetu inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, haturuhusiwi kusema nani kaitwa au kaandikiwa barua subirini kazi yetu inapokuwa tayari tunaiwasilisha bungeni

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JUNE 14 2014? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments