Baada ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuwasilisha Bungeni Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2016/2017, Wabunge walipata nafasi ya kuchangia hotuba hiyo.
Hapa nakukutanisha na Mbunge wa Kilombero Lijua Likali ambaye yeye kaguswa zaidi na hii ishu ya uhaba wa sukari..>>’Leo ajabu karibu tani 8 za sukari zilikuwa kwenye godauni liliopo Tabata, hii tafsiri yake ni kwamba kuna sukari imefichwa na wafanyabiashara‘
‘Wakati Rais anania safi ya sisi kupata sukari na viwanda viendelee wao wanaficha sukari, kibaya baada ya upungufu hawa watu wanataka wapewe vibali vya kuagiza sukari.Hawa watu kwa tabia yao ni kwamba kwa hatuna hakika kama wataagiza ambacho wameruhusiwa‘
‘Mimi huwa najiuliza, hivi nia ya Serikali kubinafsisha hivi viwanda ilikuwa ni nini? ilikuwa ni kuwapa watu nafasi ya maeneo ya kufuga ama kuongeza uzalishaji na ajira?‘
Unaweza kuendelea kwa kumsikiliza Lijua Likali hapa chini kwenye hii Video…
ILIKUPITA HII BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI ZAIDI YA BILIONI 81 ILIVYOWASILISHWA BUNGENI?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE