Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia Deodatus Thadei Luhela maarufu Baba Banzi (35) Mhasibu wa Kampuni ya kichina iitwayo ‘‘Your Home Choice’’ iliyopo Keko kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kituo cha Polisi huku akidai kuwa Majambazi walimjeruhi na kumpora Tsh 60,000,000 alizotumwa na Mwajiri wake kuzichukua kutoka Benki eneo la TAZARA.
“Tukio limetokea November 14,2022 eneo la Chang’ombe Temeke ambapo Mtuhumiwa huyo alidai tarehe hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi alikamatwa na Majambazi wawili waliokuwa na gari nyeusi baada ya kumtishia kwa silaha baadae akaingizwa kwenye gari ambapo walimjeruhi mkono wa kushoto na shavuni, na kumpora fedha alizokuwa nazo na baadae kumtupa maeneo ya Gongo la Mboto njia panda ya Pugu na Mbezi alijikongoja hadi kituo cha Polisi kidogo cha Gongo la Mboto ambako alipewa PF. 3 kwaajili ya matibabu.